0


zuma

Imekuwa ni kawaida kwa wananchi kuandamana na kupinga jambo pale wanapoona haliendi sawa ama haki haikutendeka; nchi kama  Libya, Misri, Gabon, Zimbabwe, Afrika ya Kati, Burundi na nchi nyinginezo barani Afrika zimekuwa na maandamano mara kadhaa katika kushinikiza serikali kuondoka madarakani kutokana na sababu mbalimbali.

Maandamano yanayoendelea hivi sasa Afrika ya Kusini katika Miji ya Johannesburg, Cape Town na Durban  yakiongozwa na  mashirika 75 ya kiraia kumshinikiza Rais Jacob Zuma kurejesha fedha alizotumia kukarabati nyumba yake kwa fedha za umma takribani dola milioni 17 huku wananchi wakiishi katika dimbwi la umasikini uliokithiri yasiipelekee nchi hiyo kuingia katika machafuko kama ilivyotokea Burundi.

BURUNdi 1

Mapema mwaka jana idadi kubwa ya wananchi wa Burundi walijeruhiwa na kupoteza maisha katika maandamano ya kumpinga Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kugombea Urais kwa muhula wa tatu; maandamano huko Afrika ya Kusini yanayoendelea hivi sasa yakilenga kumng’oa madarakani Rais Zuma yasijepelekea matatizo kama yaliyoikumba Burundi kwani wananchi watataabika na kuendelea kuanguka kiuchumi kutokana na maandamano hayo.

Mashirika hayo na wananchi wa Afrika Kusini wamefikia uamuzi huo kufuatia maamuzi yaliyotolewa  Machi 31na Mahakama ya Katiba, yakimtaka Rais Zuma hakufuata mapendekezo ya msimamizi wa mali za umma ya kumtaka kulipia gharama za ukarabati wa nyumba yake binafsi huko Nkandla, KwaZulu-Natal, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka katiba.

Mjini Johannesburg, mamia ya waandamanaji wakiwemo wasomi, wanasiasa, walinzi wa mazingira, wanafunzi, wafanyabiashara na wanaharakati wa kijamii wameshiriki kwenye maandamano hayo wakimtaka Rais Zuma ajiuzulu.

Post a Comment

 
Top