0

Mlinzi wa  Kampuni ya  Ulinzi ya Imara , Samwel Alcado (39) amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya chumba chake kutokana na kile kinachodaiwa ni kugundulika kuwa ana virusi vya Ukimwi (VVU).
Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mji wa Zamani Manispaa ya Mpanda amejinyonga kwa kutumia shati lake.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Margret John amesema tukio hilo  limetokea  leo  majira  saa kumi na moja alfajiri ndani ya   chumba alichokuwa  akiishi   Alcado.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli halisi wa tukio hilo.

Post a Comment

 
Top