Karibu katika mfululizo wa
makala mbali mbali makala zinazo husu ndege mbalimbali zilizopo ndani na nje ya
tanzania.Nakatika makala hii kwa siku yaleo makala ya jicho letu imeangazia
ndege jamii au aina ya Bata mzinga..........
Ndege
hawa ni wakubwa kabisa wa Phasianidae. Kichwa chao hakina manyoya
na kina rangi ya nyekundu, pinki au kijivu. Manyoya yana rangi ya nyeusi
imetayo yenye madoa. Hula makokwa,
mbegu, beri,
mizizi na wadudu, pengine amfibia na watambaachi. Jike hutaga mayai 10-14 katika shimo la kina kifupi.
Makinda hutoka tago katika masaa 12-24.
Bw. Alex juma nimfugaji maarufu wa
bata mzinga mkoani rusha anaeleza kuwa Wengi watahoji
nitafugia wapi! Hautakuwa una shida ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana
kwa kuwa mfumo wa sisi hasa watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za
kupata mwisho wa mwezi kiasi kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya
sana. Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya udanganyifu kwa kuwa
tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na mwisho wa siku ajira zetu
sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika, kuharibiana ajira.
Hii yote ni dhambi tu, hatutaki kushirikiana
ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato chetu na kufanya kazi za
umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.
Sio
mada yangu hii leo lakini naomba tujue baadhi ya sababu zinazojenga ukanjanja
kazini. Hatujipangi kikamilifu, tunacheza na majukwaa (tunataka kuonekana
na jamii tuna uwezo kumbe si kweli)
Alieleza Bw. Alex
Bata
Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15,
ni
pambo
la nyumba pia.
Kwanini
na muongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila ninapoenda katika Super Markets
kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena bei kubwa tu, mfano mimi
nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi 25,000 walikuwa watano ambayo
ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa
wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa kuanzia shilingi 10,000 na bata
mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000 hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa
kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe mkulima?
Bata
mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15 kwa dume anauzwa hivi;
Bata
mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata
mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano
una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume 1,000 unajua utakuwa una miliki
shilingi ngapi?
Ukiwa
na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi 60,000 = 60,000,000
Ukiwa
na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi 70,000 = 70,000,000
Mfano
ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata mzinga wadogo 40 kwa shilingi
25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na madume 15 kwanza ili uanze
kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza. Chukulia mfano jike moja likitotoa
vifaranga 10 x 25 = 250. Fanya kila bata mzinga atotoe mizunguko mitano
itakuwa 250 x 5 = 1,250
Sasa
chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na majike nusu 625 x 10 =
6,250. Chukua idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona
wanavyoongezeka kutoka 40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni
milionea hizi ni sawa na shilingi 467,400,000 unazo ndani.
Bata
mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu kwa nusu utapata majike 3,895
chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila mmoja utapata bata mzinga
38,950
Bi.Juliet
Mretu ni mtaalamu wa malezi ya vifaranga vya bata mzinga anaeleza kuwa ….
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza
kama vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000. 38,950 x
25,000 = 973,750,000 hii ni fedha taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.
Katika
miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea
kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa
bata.
Leo
tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa
bata mzinga 50,000.
Kazi
yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji
na fedha. Unaweza kustaafu kazi ya kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na
ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate tama.
Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza
madaraka mwaka 2005 jana tu tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka
2010 tena tumempigia kura na sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je
huoni kuwa jana tu imeshageuka leo?
Hujachelewa
bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu Januari, 2014 badilika anza
ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia nitakutafutia masoko pia, na
nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui atakayenisaidia mbele ya safari.
Ila wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika
ufalme wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.
Ushauri
wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone
kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja
maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena
elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na
vifanyiwe kazi.
uwasiliane kwa kupeana mawazo
Maoni
yako ni Muhimu sana .
Naamini kuwa umeelimika na makala hii kuhusu
ndege jamiii ya BATA MZINGA usikose kutembelea ukurasa wangu wa facbook kila
siku kwani nitakuwa nikitoa historia na maajabu ya ndege mbalimbali
duniani ..........
Mwandishi wa makala hii ni mimi
HERITENSON ELIGARD MLAY
+25573505678
Herrymlay@gmail.com
Post a Comment