Baada ya
headlines kadhaa za hivi karibuni kwa Wahisani wa Marekani na ulaya
kuripotiwa kwamba wamejitoa kuisaidia Tanzania baada ya uchaguzi wa
Zanzibar kufanyika wakati kukiwa na malalamiko, serikali ya Tanzania leo
April 4 2016 imekuja na hii.
Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile
na kufafanua kwamba kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea
kuisadia serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa
makundi 14 ya kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli.
Taarifa
hiyo imesisitiza kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya
Tanzania ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Washirika wa Maendeleo
nane waliahidi kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo
ya Afrika, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden na
Benki ya Dunia.
Kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo
wameshathibitisha kusaidia bajeti kuu ya serikali na washirika hao ni
pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja
na Benki ya Dunia ambapo washirika wengine wa maendeleo wataendelea
kuisaidia serikali kupitia mfuko wa pamoja wa maendeleo na miradi.
Washirika
hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark, Finland, Ufaransa,
Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea ya Kusini, Norway,
Sweden, Uholanzi, Uingereza, Marekani na Uswisi ambapo washirika
wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya serikali ni Benki ya
Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC
pamoja na Saudia Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.
Taarifa
hiyo ya Dkt. Likwelile imeongeza kwamba serikali ya pamoja na washirika
wa maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna
ya kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo
ambapo serikali imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea
kuisaidia Tanzania katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa
wananchi.
Post a Comment