Ilipoishia sehemu ya pili ( kama hukuisoma bofya hapa)
...Baada
ya kukamilisha yote hayo Madam Mbeshi akasogeza kiti chake karibu na
meza kisha akaketi halafu akaanza kusogeza vitu vilivyokuwepo mezani
pale lakini ghafla akakutana na karatasi chafuchafu mezani kwake lakini
ilikuwa na maandishi.
Akashtuka
kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka
kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao....
Sehemu ya pili
...Mwalimu
Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu
alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari
iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule
uliosomeka "POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO..
MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU
KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI"
Jasho
jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. Akataka
kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile
limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu
iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi
wakitembea tembea.
Madam
Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi
kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats
Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari
kwenye sumaku.
Mbeshi
alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani walizidi kumpanda
mwilini kwa kasi na kumtia ghasia. Machozi yalimtoka mwalimu mbeshi
lakini kila tone lililodondoka lilikuwa damu.
Hofu
ikamzidia sana, hakuwa na tumaini la kusalimika tena kwani kwa hatua
aliyofikia ilitisha sana. Na yote hayo yalisababishwa na binti Doreen
Mbwana.
Ghafla
mlango wa ofisi ya mwalimu Mbeshi uligongwa lakini Mbeshi hakuwa hata
na uwezo wa kuzungumza chochote. Mlango uligongwa sana lakini Mbeshi
hakuweza kuufungua ingawa alitamani yule aliyegonga mlango aingie ili
iwe ahueni kwake lakini ilishindikana.
Kila
aliponyanyua kinywa ulimi ulikuwa mzito na hakuweza kuzungumza chochote
ikambidi atulie kimya akiugulia mateso yake yalimzonga ndani ya muda
mfupi tu.
Post a Comment