15

Kuna aina nyingi za ndege aitwaye tai, mfano kuna tai mwenye mkia mweupe, kuna tai wa rangi ya dhahabu, kuna tai wa Ufilipino na kadhalika.
Inakadiriwa kufikia aina sitini za  tai duniani wengi wao wanapatikana  Afrika, Asia na Ulaya.

Tai ni ndege kama walivyo ndege wengine, ingawaje wao wana sifa za pekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, kupaa na uwezo wao mkubwa wa kuona mbali. Kwa sababu kuna aina mbalimbali, hata maumbile yao yanatofautiana. Aina ya tai mwenye uzito mkubwa kabisa ni aina ya “Steller’s sea Eagle”  ana uzito unaofikia kilogramu 6.7.

 Tai mwenye mabawa marefu kuliko wote ni aina ya “White Tailed Eagle” mabawa yake yana jumla ya urefu wa sentimita 218.5, sawa na mita 2.185. Tai aina ya “Phillipine Eagle” ndio wanaoongoza kwa urefu, wao wanafikia sentimita 100.
Pamoja na sifa hizo, tai ana mambo mengine saba makubwa tunapaswa kujifunza  katika maisha yetu. Mungu katika maandiko matakatifu anatolea mfano wa watu wanao mtegemea yeye; watakuwa kama tai. Ana sema hivi;-

“Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamgojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama TAI; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia. Isaya 40:30-31”

Ni jukumu lako kuyashika mafundisho  na kuyafanyia kazi, na ukiyazingatia vema maisha yako yanabadilika kabisa na utakuwa mwanzo mzuri kwako kuelekea mafanikio makubwa. Hebu tujifunze mambo hayo saba kutoka kwa tai.

Jambo la kwanza
Tai hupaa juu sana angani wala shomoro na kunguru hawawezi kufika huko. Hakuna ndege yeyote mwenye uwezo wa kupaa juu sana kufikia kimo anachofikia tai, labda awe tai mwenyewe. Mara nyingi huwa tunawaona mwewe wakipita sehemu fulani, shomoro na kunguru huwazomea, lakini tai hataki vurugu hizo.
Tunajifunza nini? Kaa mbali na shomoro na kunguru. Tai huruka na tai wenzake.

Jambo la pili
Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. Wanaweza kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano. Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale  na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.

Tunajifunza nini? Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame maono yako bila kuangalia pembeni mpaka uyapate au uyatimize hiyo ndiyo siri ya kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma.
Jambo la tatu

Tai hali mizoga. Anakula kile tu alichokamata yeye.
Tunajifunza nini? Kuwa makini na kile unacholisha macho yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga       (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu nafsi yako na maisha yako hayatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio.

Jambo la nne
Tai wanapenda mvua kubwa na yenye upepo.
Mawingu yakikusanyika tai wanafurahi. Tai hutumia upepo wa mvua kupaa juu sana angani hata juu ya mawingu. Akifika huko juu sana hatumii nguvu nyingi kupaa anaweza kutandaza tu mabawa yake halafu anaanza kuelea bila shida akifurahia maisha mazuri.
Huku ndege wengine wakati wa mvua kubwa yenye upepo,  hujificha kwenye mapango na kwenye vichaka.

Tunajifunza nini? Tunaweza kutumia mvua kubwa yenye upepo                (changamoto)  kujinyanyua juu sana . watu wote waliofanikiwa wengi wao hufanikiwa wakati wa changamoto kubwa. Wao hutumia mvua ya upepo kupaa juu sana angani tena wakati mwingine juu ya mawingu.

Jambo la tano
Tai hupima kwanza kabla ya kuamini.
Tai jike akikutana na tai dume na wakataka kujamiiana, tai jike hupaa kwa kasi kubwa kwenda chini wakati huo tai dume anafuatia kwa nyuma. Akifika chini huchukua tawi la mti kisha hupaa tena angani na tawi hilo huku tai dume anafuata kwa nyuma.

 Akifika umbali mrefu angani tai jike huliachia hilo tawi na tai dume hulikimbilia mpaka alikamate kabla halijadondoka chini na akisha likamata analirudisha tena  juu kwa tai jike.
Tai jike atalipokea hilo tawi na anapaa nalo juu sana halafu analidondosha tena. Kama kawaida yake tai dume atalifukuzia mpaka alikamate na atalirudisha kwa tai jike tena. 

Tai jike ataendelea na mchezo huu mpaka ajiridhishe kwamba tai dume huyo,  yuko vizuri na amefuzu majaribio hayo, hapo ndipo tai jike atakubali kupandwa na tai dume huyo.

Tunajifunza nini? Katika maisha yako binafsi au katika  biashara yako, unatakiwa kupima mtu unayetaka kushirikiana naye kama kweli amedhamiria kushiriki na wewe.  Maana wapo wengine ni waigizaji tu.

Jambo la sita
Akitaka kutaga mayai, tai jike na tai dume hushirikiana kutafuta sehemu salama iliyo juu sana kwenye mti ambayo sehemu hiyo haina maadui.

 Kisha, tai dume anaenda chini ardhini kuchukua miti yenye miiba anakuja anaitandaza kwenye sehemu wanayotengeneza kiota. Tai dume  tena, hurudi ardhini kuchukua matawi ya miti kwa jili ya kutengeneza kiota. 

Hurudia na kurudia mpaka kiota kinakuwa kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vidogo vya miti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini,  akimaliza kuweka majani laini anarudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui, na mwisho akimaliza hayo yote ana nyonyoa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai yatakapokuwa iwe laini.

Tai jike akisha taga mayai; wanasaidiana na tai dume kuyaatamia kwa zamu, pia kazi ya ulinzi huifanya wote kwa kushirikiana. Vifaranga wakishatotolewa; tai dume na tai jike hushirikiana kuwalea

. Baada ya muda kidogo tai jike ataanza kuwatoa vifaranga na kuwaweka kwenye miiba pembeni kidogo ya kiota, halafu vifaranga hurudi ndani ya kiota, atafanya hilo zoezi mara kadhaa baadae atayaondoa manyoya kwenye kiota. 

Wale watoto wakirudi kwenye kiota watakutana na miiba itawachomachoma na kuvuja damu. Kisha tai jike atawarusha chini wale vifanga;  kabla hawajadondoka tai dume atawadaka ataendelea na zoezi hilo mpaka watoto wafahamu kuruka.

Tunajifunza nini? Pale tai wanapoandaa kiota wanatufundisha kujiandaa kwa ajili ya mabadiliko. Lakini ushiriki wa mke na mume ni muhimu sana ili kujenga familia yenye mafanikio.

Tai jike anapoyaondoa manyoa kwenye kiota, anataka tujifunze kwamba kuishi kwa maisha yale yale bila kuchomwa na miiba hutapata uzoefu na maarifa ya kukupeleka kwenye mafanikio.  

Miiba ( changamoto) ndizo zinazokukomaza kwenye safari yako ya kufanikiwa. Usizilaumu changamoto bali tafuta namna ya kukabiliana nazo huku ukijifunza kitu kutokana na changamoto hizo.

Hata ukiwa na watoto wako, wakati mwingine wapitishe kwa makusudi kwenye mazingira magumu ili wajifunze kitu. Wapitishe mara kwa mara kisha unapomaliza kuwapitisha waulize wamejifunza nini?. Utakuwa unawasaidia.

Jambo la saba
Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hayatamwezesha kupaa kwa kasi kama hapo mwanzo.  

Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.

Tunajifunza nini? Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa.
 Tabia zinazotukwamisha kupaa kwa kasi kubwa ni mzigo kwetu

. Tunatakiwa kuziacha mara moja. Sio tabia tu bali hata maarifa. Huenda bado unaishi kwa kutumia maarifa ya zamani ambayo yanakukwamisha kupaa kwa kasi kubwa kwenye mafanikio yako, basi unatakiwa kujifunza maarifa mapya ili uweze kufanikiwa kwa kasi kubwa.

“Pamoja na sifa hizo, tai ana mambo mengine saba makubwa tunapaswa kujifunza  katika maisha yetu. Mungu katika maandiko matakatifu anatolea mfano wa watu wanao mtegemea yeye; watakuwa kama TAI”

Hurudia na kurudia mpaka kiota kinakuwa kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vidogo vya miti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini,  akimaliza kuweka majani laini anarudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui, na mwisho akimaliza hayo yote ana nyony

oa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai yatakapokuwa iwe laini.
Tai jike akisha taga mayai; wanasaidiana na tai dume kuyaatamia kwa zamu, pia kazi ya ulinzi huifanya wote kwa kushirikiana. Vifaranga wakishatotolewa; tai dume na tai jike hushirikiana kuwalea

. Baada ya muda kidogo tai jike ataanza kuwatoa vifaranga na kuwaweka kwenye miiba pembeni kidogo ya kiota, halafu vifaranga hurudi ndani ya kiota, atafanya hilo zoezi mara kadhaa baadae atayaondoa manyoya kwenye kiota. 

Wale watoto wakirudi kwenye kiota watakutana na miiba itawachomachoma na kuvuja damu. Kisha tai jike atawarusha chini wale vifanga;  kabla hawajadondoka tai dume atawadaka ataendelea na zoezi hilo mpaka watoto wafahamu kuruka.

Tunajifunza nini? Pale tai wanapoandaa kiota wanatufundisha kujiandaa kwa ajili ya mabadiliko. Lakini ushiriki wa mke na mume ni muhimu sana ili kujenga familia yenye mafanikio.

Tai jike anapoyaondoa manyoa kwenye kiota, anataka tujifunze kwamba kuishi kwa maisha yale yale bila kuchomwa na miiba hutapata uzoefu na maarifa ya kukupeleka kwenye mafanikio.  

Miiba ( changamoto) ndizo zinazokukomaza kwenye safari yako ya kufanikiwa. Usizilaumu changamoto bali tafuta namna ya kukabiliana nazo huku ukijifunza kitu kutokana na changamoto hizo.

Hata ukiwa na watoto wako, wakati mwingine wapitishe kwa makusudi kwenye mazingira magumu ili wajifunze kitu. Wapitishe mara kwa mara kisha unapomaliza kuwapitisha waulize wamejifunza nini?. Utakuwa unawasaidia.

Jambo la saba
Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hayatamwezesha kupaa kwa kasi kama hapo mwanzo.  

Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.

Tunajifunza nini? Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa.
 Tabia zinazotukwamisha kupaa kwa kasi kubwa ni mzigo kwetu

. Tunatakiwa kuziacha mara moja. Sio tabia tu bali hata maarifa. Huenda bado unaishi kwa kutumia maarifa ya zamani ambayo yanakukwamisha kupaa kwa kasi kubwa kwenye mafanikio yako, basi unatakiwa kujifunza maarifa mapya ili uweze kufanikiwa kwa kasi kubwa.

“Pamoja na sifa hizo, tai ana mambo mengine saba makubwa tunapaswa kujifunza  katika maisha yetu. Mungu katika maandiko matakatifu anatolea mfano wa watu wanao mtegemea yeye; watakuwa kama TAI”

Post a Comment

Top