0

Rwanda na Tanzania zimeahidi kushirikiana zaidi kibiashara katika ukurasa mpya wa uhusiano baina ya mataifa hayo jirani.

Hayo yamewadia katika mkutano wa rais wa Rwanda Paul Kagame na mgeni wake rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Marais hao wameyasema hayo leo mnamo mwanzo wa ziara ya rais Magufuli nchini Rwanda ambayo ndiyo ziara yake ya kwanza kuchaguliwa kwake mwaka uliopita.

Maneno ya undugu,urafiki ,uhusiano mwema na uhusiano imara yametamkwa sana na viongozi hawa,Rais Kagame akisisitiza ndio ndiyo msingi mkubwa wa kujenga nchi hizi mbili.

Ziara hiyo ya siku mbili inaangaliwa na wengi kama ya kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya kipindi Fulani cha uhusiano baridi.
Rais wa Rwanda Paul Kagame na mgeni wake rais wa Tanzania John Pombe Magufuli walikutana leo
''Mnajua vyema kuwa mimi sipendi kusafiri, kwa sababu ninapenda kubana matumizi.
''Nimealikwa sehemu nyingi hata ulaya nimealikwa lakini bado sijaenda.
''Lakini nilipoalikwa na rais kagame mnaona nimeshafika hapa''

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli mara tu baada ya uzinduzi wa daraja la Rusumo linalounganisha Tanzania na Rwanda ambalo amelizindua rasmi yeye na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
''Nimefurahi kwa sababu nimekuja kufungua daraja la Rusumo.
 
Viongozi hao walifungua daraja la Rusumo
''Hii ni Historia kubwa inayojengeka kati ya Tanzania na Rwanda''.
''Lakini nataka kuwahakikishia ndugu zangu wa Rwanda kuwa Tanzania itatoa ushirikiano mkubwa sana kwa nchi ya Rwanda'' alisema rais Magufuli.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akihutubia hadhira hiyo alisema
''Tunataka amani,undugu urafiki na tunataka kufanya biashara ili kila mmoja wetu aweze kupata faida''
 
Ziara hiyo ya siku mbili inaangaliwa na wengi kama ya kufungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili
Ziara hii ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya nchi yake inaangaliwa na wengi hapa Rwanda kama ya kuanza ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi mbili.
Miaka ya nyuma uhusiano huo uliingiwa baridi baada ya Tanzania kuwatimua raia wa Kinyarwanda ,kitendo kilichowakasirisha viongozi wa Rwanda.Hayo yalifwatia kipindi kigumu cha uelewano mdogo baina ya nchi mbili kuhusu swala la mgogoro wa mashariki ya Congo.
Rwanda kama nchi isiyopakana na bahari kibiasha hutegemea sana bandari ya Dar es Salam na hivi karibuni Rais Kagame alimsifu mgeni wake na kuahidi kuiga mfano wake katika juhudi za kupambana na rushwa na ufisadi.

Rais Magufuli kesho ataungana na wananchi wa Rwanda katika maadhimisho ya miaka 22 ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari kabla ya kufanya mazungumzo na wandishi wa habari akiwa pamoja na Rais Paul Kagame.

Rwanda na Tanzania zimeahidi kushirikiana zaidi kibiashara

Post a Comment

 
Top