Katika karibu kila jambo duniani, mwanadamu huhitajika kutumia akili ili kufanikiwa. Bila shaka, iwapo utatarajia wazidi watu wengine hasa katika kuwapora au kuwaibia basi utahitajika kuwa na 

ujanja zaidi. Lakini maeneo mbalimbali duniani kunao wahalifu ambao walionekana kupungukiwa.
Majuzi kwa mfano, wanaume wawili kutoka Skegness, Lincolnshire, walijipiga picha wakiimba pesa kutoka kwenye mitambo ya kucheza Kamari Bradford, Uingereza. Hawakuenda mbali, kwani

walikamatwa muda mfupi baadaye Benjamin Robinson, 30, alifungwa jela miezi 32, naye Daniel Hutchinson akahukumiwa kifungo cha miezi sita jela ambacho kimeahirishwa.