Wakati
Yanga ikishuka dimbani wikiendi hii kumenyana na Al Ahly katika mchezo
wa Klabu Bingwa Afrika, beki na nahodha wa muda wa kikosi hicho, Mtogo,
Vincent Bossou, ametamka kuwa yupo fiti kukabiliana na straika hatari wa
wapinzani wao hao, Mgabon, Malick Evouna, ambaye ndiye mchezaji hatari
kwa upande wa Waarabu hao.
Bossou
anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Yanga kitakachoanza katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, mchezo utakaopigwa
Uwanja wa Taifa Aprili 9, mwaka huu.
Bossou
ambaye amewahi kucheza soka la kulipwa Vietnam amesema kuwa licha ya
mashabiki mbalimbali kuwa na hofu na kiwango chake lakini yupo vizuri
kuhakikisha anasaidia timu yake hiyo kupata ushindi.
“Sina
hofu hata kidogo katika mchezo huo kutokana na maandalizi mazuri ambayo
tunaendelea kujipa ikiwemo ya kuingia ‘gym’ kwa ajili ya kuongeza
stamina na nguvu za kupambana kwani tunajua wachezaji tunaokutana nao
wako fiti kiasi gani,” alisema.
Al
Ahly walitarajiwa kuingia nchini usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya
mchezo huo ambao marudio yake yanatarajiwa kuwa ni kati ya Aprili 19
mpaka 20, mwaka huu.
Post a Comment