Kikosi
cha timu ya Simba kwa sasa ndiyo kinaongoza Ligi Kuu Bara kikiwa na
pointi 57 ikibakiwa na michezo sita tu kuhitimisha msimu huu ambao ambao
wamedhamiria kufanya kweli kuliko misimu miwili nyuma.
Simba
iliuanza msimu huu kwa kasi ikiwa chini ya Kocha Muingereza, Dylan
Kerr, mpaka sasa inanolewa na Mganda, Jackson Mayanja inaonekana kasi
yao hiyo imekolea kwani tangu kocha huyo akabidhiwe timu hiyo
amefanikiwa kuiongoza kushinda mechi 10 za ligi na kupoteza moja pekee.
Inaonekana
hivi; misimu miwili nyuma kipindi kama hiki cha mwezi Aprili, Simba
haikuwa katika harakati za kuwania ubingwa huku ikiziachia Yanga na Azam
zikitamba.
Msimu
wa 2013/14, mwezi na tarehe kama hizi Simba ilikuwa imecheza 24,
ilijikusanyia pointi 37, ikishika nafasi ya nne, huku ikifunga mabao 40
na kuruhusu kufungwa mabao 25.
Huku
Simba ikiwa katika hali hiyo, wapinzani wake, Yanga na Azam, walikuwa
wanakimbizana nafasi mbili za juu, Azam ilikuwa kileleni na pointi zao
56, huku Yanga ikishika nafasi ya pili kwa pointi 52. Mbeya City
iliingilia kati na kushika nafasi ya tatu kwa pointi zao 46.
Mwisho
wa msimu huo, Simba ilimaliza ikiwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 38,
ikifunga mabao 41 na kuruhusu mabao 27, bingwa alikuwa Azam.
Msimu
uliofuata nao kipindi kama hiki, Simba ilikuwa imeshacheza mechi 19
ikiwa imejikusanyia pointi 32, ikifunga mabao 25 huku ikifungwa mabao 14
na kushika nafasi ya tatu.
Ndani
ya msimu huo pia Simba ilikuwa chini ya Azam na Yanga. Yanga walikuwa
wakiongoza ligi wakiwa na pointi 40, Azam ikishika nafasi ya pili na
pointi 37.
Mwisho
wa msimu huo, Simba ilimaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 47,
ikifunga mabao 38 na kuruhusu mabao 19, bingwa alikuwa Yanga.
Utaona
tofauti ya pointi kwa kipindi hicho ilivyokuwa baina ya Yanga na Azam
dhidi ya Simba, lakini kwa sasa Simba ndiyo imeziacha timu hizo licha ya
kuwa mbele kwa michezo miwili, lakini hata kama Azam ikishinda mechi
zake hizo haiwezi kuishusha Simba, angalau Yanga kama ikishinda inaweza
kuipita Simba pointi mbili tu.
Kutokana
na takwimu hizo, msimu huu unaonekana kuwa Simba ilikuwa ikijiuliza
tangu awali ilikuwa inakosea wapi na tayari imelibaini tatizo hilo kwani
kasi yao inazitishia Yanga na Azam.
Post a Comment