Karibu katika mfululizo wa makala mbalimbali makala zinazo kupa fursa ya wewe msomaji kutambua mambo mbalimbali kuusu ndege zaainazote zinazo patikana duniani naleo tutakua tuki mwangalia au kumsoma ndege aina ya BATA ambapo nae anamaajabu makubwa usio yajua fatana nami mwandishi wako HERITENSON MLAY kuweza kutazama maajabu hayo.
Bata ni ndege wa maji wa familia ya Anatidae wenye madomo mafupi na mapana na miguu yenye ngozi kati ya vidole.
Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu.
Mabata ndiyo moja ya familia za ndege ambazo spishi zao zina uume, kwa sababu mabata wanapandana majini tu.Mabata huchanganywa pengine na aina kadhaa za ndege wa maji wasiohusiana wenye maumbo yanayofanana, kama wazamaji, vibisi, kukuziwa na shaunge.
Mwili wote wa mabata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na mabata wengi kwa wastani wana shingo fupi lakini shingo la mabata bukini na mabata-maji ni ndefu.
Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa huwa wa duara kidogo.
Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri, na kwa kawaida hurushwa nyuma kabisa ya mwili.
Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana.
Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa.
Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.
Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini. Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura, mhanga.
Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti.
Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana. Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa. Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo
Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.
Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.
Wataalamu hawakubaliana kuhusu uainisho wa mabata ndani ya familia yao. hadi kufikia hapo makala ya jicholetu kwa siku ya leo imefika tamati .nikusihi msomaji usipitwe na makalama ma ridhawa inayozungumzia aina za ndege mbalimbali huku ulimwenguni.
Kwaleo tunafika tamati hapa lakini usikose makala ijayo ambapo totakua na aina nyingine ya ndege tukimchunguza kiundani zaid
Kwamaoni na ushauri wasiliana nami
Herrymlay@gmail.com
+255763505678.
Mwandishi wa makala hii ni...................HERITENSON MLAY
.
Post a Comment