0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamisi Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gaudence Milanzi kuanzisha mchakato wa kisheria wa kupandisha hadhi Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wamimbiki kuwa Pori la Akiba ili iweze kuhifadhiwa vizuri baada ya kushindwa kujiendesha.
Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo akiwa mkoani Pwani baada ya kutembelea eneo la Jumuiya hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi katika eneo hilo ambalo ndani yake pia kuna mapito ya wanyamapori.

Post a Comment

 
Top