Home
»
BURUDANI
» “Movie ya dakika 60 tumeshindwa, je tunapokimbilia tutapaweza?”-Kitale
Muigizaji na mchekeshaji Mkude Simba ambaye wengine wanamfahamu kama Kitale kutokana kujipatia umaarufu kupitia tamthilia ya Jumba la Dhahabu, Kitale
ameamua kutumia ukurasa wake wa isntagram na kueleza mawazo yake baada
ya wasanii kushindwa kufanya vizuri kwenye movie na wengine wamerudi
kwenye tamthiliya.
“Hii ni kwa wasanii wenzangu. Soko letu la movie kipindi
Cha nyuma lilitokea kupendwa na mashabiki zetu wengi sana tena sana,
hapa kati kati kulitokea songombingo nyingi sana juu ya soko letu la
film bongo kuporomoka kutokana na kazi zetu kuwa chini ya kiwango”
“Mashabiki zetu ambao ndio wanunuzi
wa kazi zetu walihamia katika series za kikorea, Baadhi ya wasanii
waliyumba sana kutokana na tegemezi lao kubwa lilikuwa kwenye biashara
ya movie tu. Kama tutakuwa tunafuatilia vizur sasa hivi wasanii wengi
tumejikita katika TAMTHILIA (Series)”
“Shaka yangu Bongo movie tumeiuwa sisi wenyewe kutokana
na Story zetu mbovu, huku tulipokimbilia ni pagumu zaidi ya movie na
ikumbukwe kua tamthilia ni story ndefu huenda hata mwaka au zaidi ya
mwaka kutokana na ww mwenyewe upendavyo kulingana na story”
“Pia inahitaji watu wengi tofauti
na movie. Swali Langu, “Movie ya dakika 60 tumeshindwa, Je huku
tunapokimbilia tutapaweza ikiwa Tamthilia ni zaidi ya dakika 60.?”
Tusije tukaharibu kotekote tukaja kosa kote..!! Ingawaje Nina Imani
tunaweza”
Post a Comment