0


Wanapiganaji 20 wa ash-Shabab wauawa na jeshi la Somalia 
 
Wapiganaji wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab nchini Somalia wameuawa na askari wa serikali, kaskazini mwa nchi hiyo. 
 
Ismail Khalifah Shira, kamanda wa jeshi la Somalia amethibitisha habari hiyo mapema leo na kuongeza kuwa, wanachama wa kundi hilo la kigaidi la ash-Shabab, wameuawa asubuhi ya leo katika eneo la Dainunay, lililopo karibu na mji wa Baidoa. Shira ameongeza kuwa, magaidi hao wameuawa baada ya kuvamia kambi ya jeshi la serikali katika eneo hilo kwa lengo la kutekeleza shambulizi la kushtukiza, na kwamba jaribio lao lilifeli baada ya askari kufahamu mapema njama hiyo na kuwaua magaidi hao katika eneo la tukio. Hata hivyo kamanda Ismail Khalifah Shira hakutaja hasara yoyote iliyopata jeshi katika hujuma hiyo.

 Hii ni katika hali ambayo kundi la ash-Shabab limedai kupata ushindi katika hujuma hiyo. Ripoti iliyotolewa na kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu, imedai kuwa wapiganaji wa ash-Shabab wamefanikiwa pia kudhibiti kambi ya kijeshi la eneo hilo la Dainunay. Aidha limeongeza kuwa, katika hujuma hiyo askari 10 wa serikali wameuawa.
Zaidi katika kategoria hii:  

Post a Comment

 
Top