FREDERICK
Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais
John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa
Sumaye
bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya
serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga
kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.
“Wapowatawala
ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye
tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.
“Huyo
ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala
uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi
wa Habri za Siasa (TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba
ya nchi.
Amesema,
serikali yoyote inayopambana na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa
kufanya kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa wanaotawala.
Akitolea
mfano wa hatua ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge
Sumaye amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja Katiba.
“Unapoondoa
matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja
katiba. Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana haki ya kupewa
taarifa wakati wote.
“Kwa
kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa moja) wewe serikali unataka
kutoa taarifa ya Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa unayoitaka
wewe,” ameeleza Sumaye.
Kuhusu sababu iliyotolewa kwamba, matangazo hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni amesema haina mashiko.
Sumaye
amesema, hata kama matangazo hayo yatarushwa na ofisi za bunge bado,
gharama zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji kununua mitambo
pamoja na kuajiri wafanyakazi wake.
Sumaye amesema, serikali yenye demokrasia ya kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa maoni.
“Serikali
yoyote yenye utawala bora, ingependa mambo yake inayoyafanya kwa ajili
ya wananchi wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao.
“Ukiona serikali inaficha mambo yake lazima kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.
George
Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa TAPOREA amezungumzia ripoti ya hali ya
uhuru wa waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari kimataifa,
iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye
Makao Makuu yake nchini Ufaransa haipendezi.
Amesema,
ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita zaidi ya
waandishi wa habari 800 kutoka mataifa mabalimbali duniani wameuawa
wakiwa wanatekeleza kazi zao.
“Kitisho
kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini ni utamaduni mpya
ulioasisiwa na kuimarishwa na watawala wa sasa na kuvishinikiza vyombo
vya habari kutomkosoa Rais John Magufuli na serikali yake.
“Matokeo yake, vyombo vingi vya habari nchini vimelazimika kuandika habari za kumfurahisha Rais Magufuli,” amesema Maziku.
Post a Comment