0
paris-jackson-2
                               NEW YORK, MAREKANI
 MTOTO wa marehemu Michael Jackson, Paris Jackson, amesema tangu alipofariki baba yake mwaka 2009 hana mpango wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

 Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 17, amedai hana sababu ya kuisherehekea siku hiyo kwa kuwa atakuwa na machungu ya kumkumbuka baba yake.

Paris anatarajia kufikisha miaka 18 Aprili 3 mwaka huu, siku hiyo ataifanya maalumu kwa ajili ya kumkumbuka baba yake.

“Tangu baba yangu afariki sijawahi kufanya sherehe ya kuzaliwa kwangu kwa kuwa najisikia vibaya, nakumbuka miaka ya nyuma nilikuwa nafanya hivyo nikiwa na baba mara zote na ndiyo maana nimeshindwa kufanya peke yangu kwa kipindi chote.

“Wiki ijayo nitakuwa natimiza miaka 18, hivyo nimeona ni vizuri siku hiyo kuitumia kwa kumkumbuka baba yangu mpendwa, ila sina mpango wa kusherehekea tena,” aliandika Paris kwenye akaunti ya Instagram.

Post a Comment

 
Top