Bado headlines za dogo kutoka Afghanistan Murtaza Ahmadi kuzidi kupata umaarufu kupitia ubunifu wake wa kutengeneza na kuvaa jezi kwa kutumia mfuko wa rambo wenye jina na namba ya Lionel Messi anazidi kuingia kwenye headlines.
Murtaza Ahmadi aliingia
kwenye headlines baada ya picha yake kuonekana akiwa kavaa mfuko wa
rambo ambao kautengeneza kwa kuufananisha na jezi ya timu ya taifa ya Argentina huku mgongoni ukiwa na namba na jina la Lionel Messi, kitu ambacho kilimfanya aingie kwenye headlines na kiasi cha Lionel Messi kumtumia jezi aliyoisaini.
Stori mpya ni kuwa baba wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano amaeamua kuhamia Pakistan na familia yake kutokana na kuhofia mtoto wake kutekwa, Murtaza Ahmadi ndio amefanya familia yake kuhama kutokana na kuwa na umaarufu uliofanya Lionel Messi kuhaidi kukutana na mtoto huyo aliyeingia kwenye headlines kwa kuvaa jezi ya mfuko.
Post a Comment