Mgombea urais
anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump
amechukua hatua ya kushangaza akijaribu kuimarisha uhusiano uliodorora
kati yake na wakuu wa chama hicho.
Amechukua hatua hiyo siku moja baada ya kuwakera viongozi hao kwa kusema kwamba hatatii makubaliano ya kuunga mkono mgombea mwengine, iwapo yeye mwenyewe hatashinda uteuzi wa chama hicho.
Bw Trump, anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa, amekosoa kile anachosema ni juhudi zisizo za kidemokrasia za kutaka kumpkonya ushindi katika mkutano mkuu wa kuidhinisha mgombea mjini Cleveland mwezi Julai.
Post a Comment