0

Muziki wa zamani nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ulikuwa maarufu na kuweza kuwatambulisha baadhi ya wana muziki ambao hadi leo, majina yao yakitajwa heshima yao bado inadumu.

Mwanamziki Mbaraka Mwishehe kutoka mkoani Morogoro Tanzania atakumbukwa daima kwa tungo zake zenye maneno ya busara na mafunzo ambayo yanafaa hadi kizazi cha sasa.

Lakini je pamoja na kwamba alikwisha tangulia mbele za haki, wapenzi wa muziki wa dansi waliomfahamu wanamzungumzia vipi mwanamuziki huyo.

Mwandishi wa BBC ,Esther Namuhisa alifunga safari hadi mjini Morogoro ili kubaini kuhusu jambo hilo.

Post a Comment

 
Top