Yanayoendelea dhidi ya Yusuf Manji yanashabikiwa na baadhi yetu kwa
sababu wanadhani hayatawafika. Tabia ya kukomoa mtu ni tabia mbaya na
ina madhara makubwa katika nchi. Ni dhahiri kuwa Manji sasa anaonewa na
kudhalilishwa ili kumkomoa kwa sababu ambazo watawala wanazijua
wenyewe.
Wakati suala la kutumia unga lipo kortini, Serikali imeamua kumnyanganya
hisa zake za Tigo. Sio kwamba Serikali itachukua hisa Hizo, la hasha.
Ila Manji azikose tu. Unajiuliza, Serikali hii hii imeacha matapeli wa
PAP kuitwaa IPTL na TANESCO inawalipa zaidi ya tshs 300m kila siku. Leo
mpaka mahakama inatumia suo moto kurudisha suala la hisa za Manji kwenye
Tigo ambalo halina maslahi yeyote ya Taifa. Kwanini Mahakama haikufanya
suo moto kurudisha fedha za Tegeta Escrow?
Watanzania wajue tu kuwa, mwaka 2004 Serikali iliachia hisa zake 20%
kwenye Tigo kwa USD 750,000 ( vichekesho) kwa kuiuzia kampuni kutoka
Luxembourg. Badala ya Serikali kuhangaika na maafisa wake walioachia
hisa kutoka nje ya Tanzania wanahangaika na Mtanzania aliyezirudisha
hisa Tanzania.
Uhamiaji wanamwita kuhusu wafanyakazi wake wageni kana kwamba yeye Yusuf
ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni. Aliko Dangote hakuitwa uhamiaji
kwa suala la wafanyakazi wake ila Manji anaitwa.
Wakifanikiwa kwa Manji atatafutwa mwengine, Ni sawa na kula nyama ya mtu. Hutaacha.
Manji anaweza kuwa ana madudu mengi Sana, ahukumiwe kwa haki kwa makosa
yake. Asikomeshwe kwani ukomeshaji hautaishia kwake. Asionewe. Atendewe
haki.
Post a Comment