Taasisi
ya Moyo ya Jakaya kikwete kwa kushirikiana na hospitali ya BLK kutoka
India kwa mara ya kwanza imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa
kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo bila kuusimamisha moyo kwa
kutumia mashine maalumu. Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Peter Kisenge amesema…..
>>>’matibabu
haya tunatumia kama dakika 15 kwa kila mgonjwa na tumeshawafanyia
wagonjwa kama nane, ni tiba ya aina yake kabisa tukishirikiana na
wenzertu wa India, jana tu tumeokoa zaidi ya milioni 180 ambazo
zingepeleka watu nje ya nchi wakati tungeweza kufanya hapa’.
Kwa
mmujibu wa taarifa iliyotolewa inaeleza kwamba kwa siku mbili madaktari
bingwa watatoa huduma kwa wagonjwa 18 na kwa siku ya kwanza wametoa
huduma kwa wagonjwa 9.
Taasisi
kwa kuendelea kutoa huduma hii ya upasuaji mkubwa na kwa ubora zaidi,
siku ya leo imesaini hati maalumu ya ushirikiano na taasisi ya India kwa
ajili ya kuwapa mafunzo watumishi wake na kuendelea kutoa huduma ya
upasuaji huu wa moyo kwa kushirikiana na taasisi hiyo ya BLK India.
Post a Comment