Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE) kimewataka wananchi kupuuza taarifa za
upotoshaji zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini
kuhusu chuo hicho.
Akizungumza
na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof.
Emmanuel Mjema amesema tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa
kutisha si za kweli na zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho…..
>>>“Chuo
kinafanyiwa ukaguzi wa Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za
Serikali na kwa kipindi cha miaka minne tumepata hati safi (clean audit
report) kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 .” :- Prof. Mjema.
Prof.
Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku
toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja
kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.
Ameongeza
kuwa kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya
Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na
pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika. Mafanikio mengine ni
kujenga hema kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha
karakana ya vipimo na mizani chuoni hapo.
ULIIKOSA
HII YA WAZIRI WA ELIMU KWENDA MWENYEWE CHUO CHA MT. JOSEPH DSM BAADA YA
KUPATA TAARIFA ZAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Post a Comment