BUNGE limekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na watu wanaodaiwa kuwa ni madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Taarifa
hiyo inadai kuwa video iliyomuonesha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Charles Kitwanga akijibu swali bungeni Mei 20 mwaka huu,
ilihaririwa na kusambazwa na maafisa wa Bunge.
Kitengo
cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge kilitoa taarifa ya ufafanuzi
kuhusu madai ya kuhaririwa kwa video hiyo, mjini Dodoma jana.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa taarifa hizo, si za kweli na zina lengo la
kuupotosha umma, kwani ukweli ni kwamba kipindi cha maswali na majibu
bungeni, hurushwa moja kwa moja na hupatikana kupitia vituo vyote vya
televisheni, vinavyopokea matangazo ya bunge.
Post a Comment