Mwanamume mmoja amefariki wakati wa
maandamano ya upinzani katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya, watu
walioshuhudia wameambia BBC.
Hospitali moja mjini humo imethibitisha kwamba mwili wa mwanamume umefikishwa katika hospitali hiyo lakini chanzo cha kifo chake hakijathibitishwa.
Jijini Nairobi, maafisa wa polisi wametawanya waandamanaji waliokuwa wakitaka kufika katika afisi kuu za tume hiyo.
Shughuli za kibiashara katika jiji hilo zimetatizika pakubwa.
Polisi wamekuwa wakikabiliana na makundi ya wafuasi wa muungano huo wa upinzani wa Cord kwa mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Maandamano pia yameshuhudiwa katika miji mingine kama vile Mombasa na Kakamega.
Viongozi wa CORD wanasema mmoja wa maseneta wa muungano huo amekamatwa wakati wa maandamano ya leo mjini Kakamega, magharibi mwa Kenya.
Leo imekuwa wiki ya nne ya maandamano hayo ya upinzani.
Wiki iliyopita, polisi walikabili vikali waandamanaji na baadaye walishutumiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa kutumia "nguvu kupita kiasi”.
Rais Uhuru Kenyatta wiki jana alisema upinzani unafaa kutumia utaratibu uliowekwa kikatiba iwapo unataka kufanikisha mabadiliko katika tume ya uchaguzi.
Ametoa wito kwa “upinzani kuonesha siasa komavu badala ya kutumia njia haramu kuvutia hisia.”
Post a Comment