
Mabingwa watetezi
wa kombe la klabu bingwa Afrika katika kandanda klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya
Wydad Casablanca ya Morocco katika jitihada zake za kuhifadhi taji
lao.
Mazembe inawakaribisha mabingwa hao wa Morocco katika mkondo wa pili jumatano hii.
Hii ndio itakayokuwa mara ya kwanza kwa mechi za klabu bingwa kuchezwa katikati ya juma.
Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa mkondo wa pili.
Zamalek ya Misri itakwaruzana dhidi ya Mouloudia Bejaia ya Algeria.
Aidha Zesco United ya Zambia inaialika Stade Malien ya Mali.
Zesco iko kifua mbele kwa mabao 3-1.
Vile vile mabingwa wa mwaka wa 2014 Entente Setif, ya Algeria waliotoka sare ya 2-2 na Al Merreikh katika mkondo wa kwanza sasa wanawapokea mabingwa hao wa Sudan.
Post a Comment