Balotelli alinunuliwa na Liverpool 2014
Mshambuliaji wa
Italia Mario Balotelli amesema hataki kurejea klabu yake ya Liverpool
baada ya kipindi chake cha mkopo klabu ya AC Milan kumalizika mwisho wa
msimu huu.
Balotelli amehangaika na amefunga mabao matatu pekee katika mechi 19 alizocheza.
Hata hivyo, alicheza vyema sana mechi mbili za karibuni zaidi.
"Ninataka kusalia Milan kwa sababu sikuwa na raha Liverpool na sitaki kurudi huko,” amesema Balotelli.
Mchezaji huyo, ambaye aliwahi kuchezea Manchester City, alianza kwenye kikosi cha Milan kilichopata ushindi wa 1-0 ugenini Sampdoria Jumapili.
Alihifadhi nafasi yake licha ya kuchapwa nyumbani 2-1 na viongozi wa ligi Juventus mechi iliyotangulia.
Balotelli alifunga bao moja pekee Ligi ya Premia akichezea Liverpool baada ya kununuliwa £16m kutoka Milan Agosti 2014.
Post a Comment