Messi alifunga bao lake la 500
Miamba wa Uhispania
Barcelona wamepokezwa kichapo cha tatu mtawalia La Liga baada ya
kulazwa na 2-1 Valencia kwao nyumbani Jumapili.
Kitulizo pekee kutoka kwa mechi hiyo ni kwamba mshambuliaji wao matata Lionel Messi alifunga bao lake la 500.
Ivan Rakitic aliingiza wavuni krosi iliyotoka Guilherme Siqueira na kuwapatia Valencia uongozi wa kushangaza.
Santi Mina baadaye alifunga bao la pili dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.
Barcelona sasa wanaongoza ligi kwa kuwa wamefunga mabao mengi kushinda Atletico Madrid.
Barca wana alama 76 na tofauti ya mabao 59 nao Atletico wana alama sawa lakini tofauti ya mabao 41.
Real Madrid wamo nambari tatu na alama 75 na mabao 68. on goal difference.
Walianza kwa kushindwa na Real Madrid kwenye El Clasico.
Aidha, Atletico waliwaondoa kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wiki iliyopita.
Barca huenda wakaondolewa kileleni iwapo watashindwa kupata ushindi ugenini Deportivo La Coruna Jumatano.
Atletico watakuwa ugenini Athletic Bilbao siku hiyo nao Real Madrid nyumbani dhidi ya Villarreal.
Post a Comment