Bondia aliyejiuzulu Nick Blackwell
amesema kuwa Chris Eubank jr na babaake hawana utu kulingana na vile
walivyofuatilia jeraha lake baada ya pigano.
Eubank alifanya mkutano na wanahabari baada ya pigano hilo la uzani wa kati ,wakati Blackwell alipokuwa hospitalini.
''Familia yangu na marafiki waliwataka kutozungumza lakini walikataa'',Blackwell aliliambia gazeti la the Sun.
''Nilikuwa sina fahamu na waliendelea na kuitisha mkutano na vyombo vya habari''.
'Nimeonyeshwa kanda ya mkutano huo wa vyombo vya habari na najua kilichofanyika,si utu walivyofanya''.
Blackwell aliamka wiki moja baadaye bila ya kuhitaji upasuaji.
Post a Comment