Kiongozi wa mrengo
wa kushoto nchini Afrika Kusini Julius Malema ameonya kuwa chama chake
kitamzuia Rais Jacob Zuma kuhutubia bunge kufuatia uamuzi ulitolewa na
mahakama ya juu zaidi nchini humo kuwa alikiuka katiba kwa kukataa
kuilipa serikali pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi.
"Kati ya sasa na wakati wa kumuondoa madarakani, Rais hatuzungumza bungeni. Tutamzuia.Tutamsukuma." Malema alismema.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Mahakama ilisema kwa wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atalipa yenye mwenyewe.
Post a Comment