Waziri wa mashauri
ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry ameahidi kuisaidia Nigeria
kurudisha pesa za serikali zilizoibiwa na kufichwa kwenye benki za
Marekani.
Taarifa zinasema kuwa maafisa wa Marekani watakutana na kitengo cha kupambana na ufisadi cha Nigeria kuzungumzia zaidi suala hilo.
Bwana Buhari amechukua msimamo mkali dhidi ya ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu aingie ofisi mwaka uliopita.
Post a Comment