Mashirika ya
kifedha ya kigeni nchini Zimbabwe yametoa mipangilio ya kugawa umiliki
wao kwa wenyeji wa zimbabwe, baada ya onyo la serikali kuwa huenda
yakafungwa ikiwa yatashindwa
kufanya hivyo kabla ya tarehe ya mwisho ya
hii leo kwa mujibu wa gazeti la serikali la the Herald.
Sera hiyo
inahitaji mashirika ya kigeni kusalimisha asilimia 50 ya hisa kwa
wenyeji ambapo mashirika ya kifedha, viwanda na madini yakiwa ndiyo
yanalengwa.Kuna wasi wasi mkubwa miongoni mwa raia wa Zimbabwe kuwa viwango vya sasa vya juu vya ukosefu wa ajira huenda
vikaongezeka zaidi ikiwa serikali itaendelea na mipango yake ya kufunga makampuni ya kigeni ambayo yameshindwa kutekeleza sera
hiyo.
Makampuni ya kigeni yaliyo nchini Zimbabwe ni pamoja na kutoka nchini Uingereza, Afrika Kusini na China.
Post a Comment