0

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo Mei 3 2016 kwa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kushuka katika uwanja wa Kambarage Shinyanga kucheza na wenyeji wao Stand United Chama la wana, huu ulikuwa ni mchezo wa 27 wa Ligi kwa Yanga.

Yanga leo Mei 3 2016 wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli ya Yanga yalianza kufungwa dakika ya pili na Donald Ngoma na dakika 42 baadae Ngoma akapachika goli la pili kwa Yanga kabla ya dakika ya 63 Amissi Tambwe kuhitimisha idadi ya magoli kwa Yanga kwa kupachika goli la tatu lililowafanya Yanga wafikishe jumla ya point 68.

Goli pekee la Stand United lilifungwa na Elias Maguli dakika ya 82 kwa mkwaju wa penati, hiyo ilikuwa ni baada ya Thabani Kamusoko kufanya faulo ndani ya eneo la hatari, kwa upande wa mshambuliaji wa Yanga Ammisi Tambwe aliyekuwa na goli 19 amefanikiwa kuvunja rekodi yake aliyoiweka ya kufunga magoli 19 katika Ligi Kuu Tanzania akiwa na Simba, hiyo inatokana na leo kufanikiwa kufunga goli la 20.

Post a Comment

 
Top