0


Polisi ya Misri yakamata mamia ya watu wanaopinga kukabidhiwa Saudia visiwa viwili
Polisi ya Misri imewatia mbaroni mamia ya waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Abdel Fattah el-Sisi wa nchi hiyo ya kuipatia Saudia visiwa viwili ambavyo ni mali ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Kwa mujibu wa duru za habari nchini Misri, polisi imewatia mbaroni karibu watu watu 250 kwa tuhuma za kufanya maandamano hayo yaliyopigwa marufuku na serikali. Kamisheni ya kutetea haki na uhuru nchini Misri imetangaza leo kuwa, polisi hiyo imewakamata watu hao katika maeneo tofauti na kwendanao kusikojulikana. Imeongeza kuwa, watu 19

 miongoni mwa watu hao walioshikiliwa na polisi wa Misri ni waandishi wa habari na 40 wakiwa ni wanawake. mji wa Cairo ndio umetajwa kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliotiwa mbaroni ikilinganishwa na mikoa mingine ya nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo Jumatatu ya jana kijana mmoja aliyekuwa katika maandamano hayo mkoani Alexandria, alipoteza maisha baada ya

kukanyagwa na gari ya polisi. Mauaji ya kijana huyo yalitajwa kuwa ya kwanza katika harakati za kupinga hatua ya Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri ya kuipatia Saudia visiwa viwili vya Tiran na Sanafir vilivyoko katika Ghuba ya Aqabah.

Post a Comment

 
Top