0
Salma Said
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ya Dar es Salaam, limesema Mwandishi wa Habari wa DW na Mwananchi, Salma Said anayedaiwa kutekwa alisema alipita lango namba mbili huku kamera za CCTV   zikionyesha kuwa alipita lango namba moja.
Akizungumza   Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa kauli ya mwandishi huyo inakinzana na taarifa  iliyorekodiwa katika kamera.
Alisema  kamera hiyo ilionyesha kwamba baada ya mwandishi huyo kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), alikuwa akitembea katika maeneo mbalimbali ya uwanja huo.
“Kwa sasa tunaendelea na upelelezi  kujua mwenendo mzima wa tukio hilo  na  ukikamilika tutatoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa sababu hatutaki kumuonea mtu tunapenda kila mwananchi apate haki yake,” alisema Kamanda Sirro.
Salma  alitekwa Machi 18 mwaka katika uwanja huo  wakati akitokea Zanzibar na siku tatu baadaye  alikutwa katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Salma alipohojiwa na vyombovya habari,  alidai kwamba alitekwa na wanaume wawili  baada ya kumkamata na kumuingiza kwenye gari na  kuondoka naye kusikojulikana.
Alieleza kuwa watu hao walimfunga mtandio wake  mweusi usoni   asibaini mahali walikokuwa wakimpeleka.

Post a Comment

 
Top