0


Marekani imepora dola bilioni 2 za Iran: Zarif 
 
Hatua ya mahakama moja ya Marekani kutoa hukumu ya kuchukua udhibiti wa dola bilioni mbili za Iran zinazozuiliwa nchini humo ni sawa na uharamia. 
 
Katika mahojiano na gazeti la The New Yorker siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria hukumu hiyo ya mahakama ya Marekani na kusema: "Huo ni wizi. Ni wizi mkubwa. Ni uharamia. Hakuna shaka tutachukua tena udhibiti wa fedha hizo."

Siku ya Jumatano ya tarehe 20 mwezi huu, Mahakama Kuu ya Marekani ilipitisha uamuzi kuwa katika kuchunguza madai ya waathirika wa eti makosa ya jinai za ugaidi mahakama za nchi hiyo zinaweza kutumia mali na fedha za Iran zilizozuiliwa nchini humo ili kuwalipa fidia watu hao.

Mahakama hiyo ilisema dola bilioni mbili za Iran zilizo katika banki za Markenai zipewa familia za wanajeshi wa Marekani waliouawa mwaka 1983 katika hujuma ya bomu Beirut ambayo Iran

inatuhumiwa kuhisika nayo. Iran imekana vikali kuhusika na hujuma hiyo na kusema fedha ambazo mahakama ya Marekani imezichukua ni mali ya Benki Kuu ya Iran. Fedha hizo zilikuwa zinashikiliwa na Marekani kutokana na vikwazo dhidi ya Iran. Zarif amekosoa vikali mahakama za Marekani na kusema zimepoteza itibari. Ameongeza kuwa ni mahakama hizo hizo ndizo ambazo
zilidai mwezi uliopita kuwa eti Iran ilihusika na hujuma za Septemba 11 mwaka 2001. Katika

hukumu hiyo, mahakama moja ya New York iliamuru Iran ilipe fidia ya dola bilioni 11 kwa familia za waliopoteza maisha katika hujuma za 9/11. Zarif ameshangaa ni vipi Iran inalaumiwa kuhusika na hujuma za 9/11 wakati wahusika wakuu wanaondolewa hatiani. Itakumbukwa kuwa Marekani

imekataa kutangaza hadharani kurasa 28 za ripoti ya Tume ya Kuchunguza Matukio ya 9/11 ambayo ina ushahidi wa wazi kuwa Saudi Arabia ilihusika na mashambulio hayo ya kigaidi.

Zarif aidha amesema kuwa Iran haitafanya mazungumzo kuhusu uwezo wake wa kujihami. Amesema Iran haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani kuhusu uwezo wake wa makombora.

Post a Comment

 
Top