Kwa tamaduni nyingi za kienyeji za kaskazi ya mbali sana kunguru, spishi kubwa hasa, wamekuchwa kama viumbe vya kirobo au miungu. Katika Afrika Waxhosa wa Afrika Kusini
Kwamujibu wa nyanzo vya habari vyakuaminika vina eleza kuwa Huko Marekani kunguru huwindwa kwa kibali cha serikali.
Isipokuwa kwanzia Agosti mpaka Machi, msimu wa uwindaji kunguru sababu huwa wengi na hapo watu huruhusiwa kuwinda kunguru.
Huko Uingereza ni marufuku mpaka pale mtu atakapopewa kibali.
Lakini kwatanzania ni marachache sana kukuta watu wakiwinda kukuru kulinganisha na wanyama wa misituni
Mtaalamu wa misitu ambae pia amesomea tabia za ndege mbalimbali Bw.Erasto joeli kutoka Arusha anaeleza kuwa Kunguru anamaamuzi ya haraka sana, na anamacho yenye uwezo mkubwa wa kuona, pia kunguru anaonekana kuwa na ujasiri mkubwa hamwogopi binadam wa kike (mwanamke)
Kunguru hutoa milio mbalimbali. Suala kwamba kuna mawasiliano ya kunguru ni aina ya lugha ni mjadala mkubwa mpaka leo. Kunguru pia wamejifunza kuitika milio ya wanyama wengine na tabia hii hubadilika kwa misimu kadhaa.
Milio ya kunguru ni tata na migumu kuelewa, na milio yao hutofautiana kwa spishi tofauti na hasa ugumu wa kujifunza milio huja pale ambapo inafahamika kuwa kunguru wanauwezo wa kusikia sauti ndogo sana ambazo binadamu hawezi kuzisikia.
Kunguru aina Hooded Crow ya akitafuta chakula
baada ya kutoboa
mfuko
Kama kundi, kunguru wameonekana kuwa na akili sana na majaribio mbalimbali yamethibitisha hili. Kunguru wamepata alama za juu sana kwenye tafiti za awali. Kunguru wa huko Israeli wamejifunza kutumia vipande vya mkate kama chombo cha kuvulia samaki. Spishi moja,
New Caledonian Crow, wamefanyiwa tafiti sana kutokana na uwezo wao wa kutengeneza zana za matumizi ya kila siku. [1]. Ujuzi mwingine ni ule wa kuangusha mbegu ngumu kwenye barabara inayopitisha magari makubwa ili yapasue, na kisha kusubiri taa za barabarani kuruhusu watu wapitie watawanye mbegu hizo.
Na tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa kunguru wana uwezo wa nyuso za watu.
Tangu miaka mingi wataalamu hawakubali kuhusu undugu wa familia Corvidae na jamaa yake. Mwishowe ilionekana kwamba kunguru wametokana na wahenga wa kiaustralasia na walitawanyika duniani kote. Majamaa yao ya karibu sana ni ndege wa peponi (birds of paradise), mbwigu na Australian mudnesters.
Kumbukumbu ya visukuku vya kunguru (mifupa yao) inaonyesha kwamba walikuwa wengi sana Ulaya lakini husiano baina ya kunguru wa kabla ya historia hazieleweki vizuri.
Kunguru wa makubwa ya jackdaw, kunguru rangi-mbili na kunguru domo-nene wanaonekana kuwa walikuwepo tangu zamani sana.
Kunguru waliwindwa na binadamu hadi enzi ya chuma, kitu ambacho kinaonyesha mabadiliko ya spishi za kisasa. Kunguru wa Marekani hawana historia sahihi inayoaminika. Chakushangaza spishi nyingi zimekwisha hivi sasa baada ya uvamizi wa binadamu, katika visiwa kama Nyuzilandi, Hawaii na Grinlandi hasa.
Ndege hao walichunguzwa walipokua wakitumia midomo yao
kuchukora chakula kilichokua kimefichwa kati kati ya mbao.Awali ujuzi huu ullibainika
kwa ndege wanaotunza kwenye maabara .
matokeo ya uchunguzi uliochapishwa kwenye jarida la Open
Science, yanasema kuwa kipaji hiki ni sehemu ya tabia asilia ya ndege.
Mwaka 2002, kunguru mwitu anaetunzwa kwenye maabara ya
New Caledonian crow - kwa jina Betty - aliwashangaza wanasayansi.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford walimpatia chakula
katika kikapu kisichoweza kufikiwa kwa urahisi.
Kukifikia , ndege huyo alipindisha kipande cha waya hadi
ndani ya kikapu. Ilikua ni mara ya kwanza kwa ujuzi huo wa kutengeneza kifaa
kuwahi kushuhudiwa katika ulimwengu wa wanyama.
Betty alikufa mwaka 2005, lakini baada ya miaka, hatimae
uchunguzi ulifanikiwa kurudiwa katika ndege mwingine alieko kwenye maabara.
Mkuu wa uchunguzi huo Dr Christian Rutz, kutoka chuo
kikuu cha St Andrews cha Scotland, anasema : "ilionekana ni kama ni kitu ambacho ndege
yule alikivumbua katika maabara ."
Naamini kuwa umeelimika na makala hii kuhusu ndege jamiii
ya KUNGURU usikose kutembelea ukurasa wangu wa facbook kila siku kwani nitakuwa
nikitoa historia na maajabu ya ndege
mbalimbali duniani ..........
Mwandishi wa makala hii ni mimi
HERITENSON ELIGARD MLAY
+25573505678
Herrymlay@gmail.com
Post a Comment