Watu
wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi
mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye
harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka
Said.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Augustino Senga alisema jana kuwa
tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa 5:30 usiku katika Mtaa wa
Kigala Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela. Alisema katika tukio hilo
polisi walikamata silaha moja na risasi 21.
Senga alisema majambazi hao waliokuwa wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 hawajafahamika majina wala makazi yao.
“Baada
ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuwapo kwa majambazi
yanayokusudia kuvamia kwa mfanyabiashara huyo, tuliweka mtego eneo la
tukio ndipo majambazi hayo yalikuja yakiwa kwenye gari jeusi majira ya
saa tano usiku,” alisema Senga.
Katika
tukio jingine, Wakazi wa stendi mpya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu,
Daudi Joseph (32) na Magashi Mzee wameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na
wananchi baada ya kudaiwa kuwatapeli wafanyabiashara wa ng’ombe.
Tukio hilo lilitokea Mei 5, saa saba mchana katika mnada wa mifugo uliopo Kijiji cha Maligisu wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza.
Senga
alisema walichukua fedha kwa wafanyabiashara hao wa mifugo wakidai
kuwauzia ng’ombe, lakini badala yake walitokomea pasipo kufanya hivyo.
Wakati huohuo, watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka na kupora fedha ambazo haijajulikana kiasi chake.
Senga alisema tukio hilo lilitokea katika Kata ya Kishiri, wilayani Nyamagana.
Alisema watu hao walivamia duka hilo linalomilikiwa na Phares Grabriel (56).
Senga
alisema pia walivamia duka la jirani la Revocatus Phares(28) na kuiba
kompyuta mpakato, simu moja na kutokomea na pikipiki.
Post a Comment