0


Kipa  wa zamani wa Simba, Denis Richard ambaye ni mmoja wa makipa kinda wanaochipukia, amefungiwa miaka 10 na kutakiwa kutoa faini ya Sh milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kupanga matokeo.

Richard sasa ni kipa wa Geita Gold Mine na amefungiwa baada ya kwenda chooni kwa zaidi ya dakika 15 wakati Geita ikiwa inaivaa JKT Kanembwa katika mechi ya mwisho ya Ligi Daraja la Kwanza wakati mechi ilipoisha kwa Geita kuitwanga Kanembwa kwa mabao 8-0 na kufanikiwa kupanda daraja, yaani Ligi Kuu Bara.

Lakini Richard amepatikana na hatia kwa kuwa alichelewesha mpira kuendelea ili mechi nyingine ya kundi hilo iliyotakiwa kwisha sawa kati ya Polisi Tabora Vs JKT Oljoro iliyokuwa inachezwa mjini Tabora.

Imeonekana Richard alikaa chooni muda mrefu kwa makusudi. Hivyo anahusishwa kuwa sehemu ya upangaji matokeo.

Post a Comment

 
Top