0


                     
                                             
                                                                 NATO
Mabalozi kutoka nchi za NATO watakutana na ujumbe kutoka nchini Urusi mjini Brussels kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka miwili.

Mkutano kati ya Urusi na NATO ulifutiliwa mbali baada ya Urusi kulimega eneo la Crimea mwaka 2014. Mapigano mashariki mwa Ukrain nayo yalichangia msukosuko zaidi.
 
                                Urusi ilimega eneo la Crimea kutoka Urusi mwaka 2014
Msemaji wa NATO anasema kuwa mkutano huo haumaanishi kuwa mambo yamerejea kawaida lakini ni ishara kuwa mazungumzo yanahitajika.

Mkutano huo unafanyika baada ya visa kadha katika bahari ya Baltic ambapo Marekani ililalamika vitendo vya ndege za jeshi la Urusi.

Urusi ilikana kuvunja sheria yoyote na kudai kuwa kuwepo kwa NATO mashariki mwa Ulaya sio hatua iliyo nzuri.

Post a Comment

 
Top