Klabu ya soka ya
Azam FC imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya
kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua
ya 16 Bora kwenye mechi iliyoandaliwa mjiniTunis, Tunisia.
Mabao ya Esperance yalifungwa na wachezaji Saad Bguir dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 19, Dakika ya 63.
Haithem Jouini alifunga kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula kufuatia krosi ya Hoiucine Regued na dakika ya 80, Fakhreddine Ben Youssef akafunga la tatu akimalizia pasi ya kiungo Driss Mhirsi.
Post a Comment