Wakili Jerome Msemwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti Kamati ya Nidhamu, (kushoto) akiwa na Kassim Dau, mjumbe wa kamati hiyo wakati wakitangaza matokeo ya mwisho ya kamati yao jijini Dar es Salaam, leo. |
Kamati
ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya
Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la
upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes
League).
Akisoma
hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa vilabu na wenyeviti
wa vya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa jana, Wakili Msemwa amesema
adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi
ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi.
Klabu
za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora)
zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa
daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao.
Upande
wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka
kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho
katika msimamo wa kundi lake, Kundi C.
Kamati
ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi
wa mchezo kati ya JKT Kanembwa FC v Geita Gold, Saleh Mang’ola na
kamisaa wa mchezo huo Moshi Juma baada ya kukutwa na hatia ya upagaji
matokeo.
Aidha
kamati pia imemkuta na hatia kocha msaidizi wa klabu ya Geita Gold,
Choke Abeid na kumfungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu. Magolikipa
Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold
wamefungiwa miaka 10 kutojihusisha na mpira wa miguu sambamba na kulipa
faini ya shilingi milioni kumi (10,000,000) kila mmoja.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge,
Mwenyekiti wa klabu ya Geita Gold, Cosntantine Moladi na Katibu wa klabu
ya JKT Kanembwa Basil Matei wameachiwa huru na Kamati ya Nidhamu baada
ya kutokutwa na hatia katika shauri hilo.
Mwenyekiti
wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa
chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa
klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora,
Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.
Mwamuzi
wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi
wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi
kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni
(10,000,000) kumi kila mmoja.
Katibu
wa klabu ya Polisi Tabora, Alex Kataya, Katibu wa klabu ya JKT Oljoro,
Hussein Nalinja, mtunza vifaa wa klabu ya Polisi Tabora, Boniface Komba,
na Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Mrisho Seleman, wameachiwa huru na
Kamati ya Nidhamu ya baada ya kutokutwa na hatia.
Kutokana
na maamuzi hayo ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, Kamati husika zitakaa
kupitia Kanuni na kutangaza timu itakayopanda Ligi Kuu (VPL) msimu ujao
na timu zitakazopanda Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes) msimu ujao.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA TFF, BARAKA KIZUGUTO
Post a Comment