Nyumba
ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es
salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa
moja na nusu.
Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa.
Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa.
Baada
ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu
pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob
alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi.
”Tumeshaangalia
mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila
tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala
hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika
kuangalia mazingira” amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.
Meya
alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata
nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegundua wanachama
hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.
Wema alipohojiwa amesema, ”
Mama yangu ameteseka usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa
hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana
mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushie na mabaya
yote,”.
Post a Comment