Wezi Wamchakaza Dogo Janja ....Ashitaki Kwa Paul Makonda
Rapper Dogo Janja amekumbana na janga zito.
Hitmaker huyo wa ‘Kidebe’ usiku wa kuamkia leo ameibiwa baadhi ya vitu kwenye gari lake aina ya Porte ikiwemo taa, radio na power window. Baada ya kukutana na janga hilo Dogo Janja amemuandikia ujumbe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram unaosemeka:
Muheshimiwa makonda tunashkuru umelisimamia vizur swala la madawa ya kulevya na tumeona matunda yake..lakin bado kuna hili la hawa wezi wa vipuli vya magari km taa radio powerwindow naona km alijaongelewa ivi..awa jamaa wapo wengi sana mjini na wanajulikana..wanakuibia alafu wanakupigia cm wapi pakuvipata vitu vyako..mueshimiwa tuanzishe na kampeni hii tupunguze kutiana hasara..kigali changu chenyewe ndio hiki nataftia riziki jana ucku wamekuja wameiba kila kitu radio taa za mbele na nyuma..ntatokaje kujitaftia rizik? Cc: @paulmakonda.
Post a Comment