Jeshi la Nigeria
limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la
Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya
msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa
Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.
Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka
nchi z
a Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar ameiambia BBC kuwa kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.
“Ndiyo tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote pia. Ni mtu mhimu sana katika makundi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.

Post a Comment