Home
»
HABARI
» KIGOGO WA TIC ALIYESUSIA MISHAHARA MIAKA MITATU AJILIPA KWA NAMNA HII
Moja kati ya mambo ambayo Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Nyerere aliyasimamia kidete na kuyakemea kwa nguvu zote
ni rushwa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma na ufisadi.
Katika Awamu ya Tano ya uongozi
tuliyonayo sasa kila kiongozi amekuwa na staili yake ya kutawala;
Mwalimu Nyerere alihimiza Sera ya Ujamaa akaja mzee ruksa (Ally Hassan
Mwinyi) kisha mzee wa Uwazi na Ukweli (Benjamin Mkapa) pia akaja Maisha
Bora kwa Kila Mtanzania (Jakaya Kikwete) na sasa mzee wa Hapa Kazi Tu John Pombe Magufuli kwa hakika tunaona mambo mengi.
Imepita miaka mitatu tangu Juliet
Rugeiyamu Kairuki achaguliwe kushika Wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ambaye ni Mwanasheria mwenye Shahada
ya Kwanza na ya Uzamili kwenye Sheria akiwa na utaalamu wa miradi ya
ubia kati ya serikali na sekta binafsi.
Julieth anadaiwa kujilipa POSHO
ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwa mwezi kwa madai ya kufidia mshahara
mnono aliokuwa akilipwa huko South Afrika japokuwa ukweli halisi wa
mshahara aliokuwa analipwa kabla ya kuja Tanzania ni Dola za Kimarekani
9,260 na si 15,000 kama alivyodai analijitetea Julieth.
Cha kushangaza zaidi Juliet amedaiwa
kutochukua mishahara serikalini kwa takribani miaka mitatu tangu
aajiriwe huku akiendelea kujineemesha kwa posho hizo jambo lililopelekea
leo hii Rais Dk. Magufuli kutengua uteuzi wake kwa kile alichodai
mshahara hautoshi.
Mambo haya yanatokana na Utawala wa
Serikali ya Awamu ya Nne uliowapa mwanya wafanyakazi wa umma uhuru
mkubwa uliopelekea kufanya ufisadi wa kutisha kwa kujilimbikizia mali na
kufanya matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za umma.
Post a Comment