0

Raia 16 wa Misri wauawa kwa kupigwa risasi Libya 
 
Duru za habari nchini Libya zimeripoti kuuawa raia 16 wa Misri kufuatia ufyatulianaji risasi na wafanya biashara ya magendo katika eneo la Bani Walid kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa habari hiyo raia hao wa Misri waliokuwa wanakusudia kuhajiri kinyume cha sheria kuelekea Libya na kisha Ulaya, wameuawa baada ya kupigwa risasi na wafanyabiashara ya magendo katika eneo hilo.

 Wakati huo huo, Ahmed Abu Zeid, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ameutaka ubalozi wa nchi yake huko Libya kufanya mawasiliano na viongozi wa eneo la Bani Walid na pia serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya ili kufahamu kiini cha kujiri tukio hilo. Abu Zeid pia ameutaka ubalozi huo kuchukua hatua za haraka ili kufahamu utambulisho wa wahanga wa mauaji hayo na kuirejesha miili yao nchini kwao.

Hii ni katika hali ambayo mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Mataifa nchini Libya, Martin

Kobler amelaani mauaji dhidi ya raia hao wa Misri na kutaka kufanyike uchunguzi wa haraka kubaini wahusika, kama ambavyo pia ametaka kurejeshwa utawala wa kisheria katika eneo la Bani Walid. Itafahamika kuwa raia wengi wa Misri wapo nchini Libya wakishughulisha na kazi mbalimbali. Wengi wa Wamisri hao wanafanya kazi za ujenzi nchini humo.

Post a Comment

 
Top