0


Donald Trump: Siasa za kigeni za Marekani ni msiba 
 
Donald Trump, mgombea wa nafasi ya urais wa chama cha Republican nchini Marekani amezitaja siasa za kigeni za nchi hiyo kuwa ni msiba mkubwa na zilizokosa mwelekeo au mwanga wa stratijia. 
 
Trump aliyasema hayo jana na kudai kuwa, endapo atachaguliwa kuwa rais wa Marekani atazifanya siasa za kigeni za nchi hiyo kuwa kipaumbele cha kwanza katika uongozi wake. Trump aliyasema hayo baada ya kupata ushindi katika mchuano wa ndani ya chama chake katika majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

 Amesisitiza kuwa siasa za kigeni za Marekani zitapewa nafasi kubwa katika utendaji kazi wake huku akidai kuwa, sasa umewadia muda wa kuzifanyia mabadiliko siasa hizo za kigeni nchini Marekani. Kadhalika amesema kuwa, katika kudhamini usalama wa Marekani, waitifaki wakei lazima wamudu gharama kubwa katika suala hilo.

 Amesema pia kwamba, mahusiano ya kibiashara baina ya Marekani na China lazima yafanyiwe mabadiliko na kuwepo usawa zaidi katika uga huo.

Katika sehemu nyingine ametaka kutumiwa ukandamizaji zaidi katika kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi na kusisitiza kuwa kwa kuzingatia kuwa atakuwa mtekelezaji wa sheria kwenye utawala wake, basi atapanua wigo wa sheria ya kuwahoji watuhumiwa wa uhalifu.

Post a Comment

 
Top