0



Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA), kimepiga marufuku kwa mashabiki wa Toto African na wale wa Yanga kuvamia uwanja baada ya mechi.

Yanga itakuwa mgeni wa Toto African katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

MZFA imepiga marufuku ili kuhakikisha usalama wa wachezaji na pia kufuata utaratibu.

“Wadau lazima waheshimu hili agizo, wahakikishe hawaingia uwanjani. Si jambo zuri, kila mtu abaki alipokaa,” alisema Katibu Mkuu wa MZFA, Nasib Mabruk.

“Utaona Tanga wamepata adhabu, sisi tusingependa wabaki watakapokuwa wamekaa.”

Post a Comment

 
Top