Maafisa wa usalama walianza kushika doria mapema asubuhi jumba la Anniversary Towers, lililo na afisi za IEBC
Viongozi wa Cord wakiongozwa na waziri mkuu wa
zamani Raila Odinga na waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni Moses
Wetangula walifika mwendo wa saa tano wakiandamana na mamia ya wafuasi
lakini maafisa wa usalama wakawazuia kuingia katika afisi hizo. Mrengo huo unataka viongozi wa tume hiyo waondolewa.
Wanasema viongozi hayo hawawezi kutegemewa kuendesha uchaguzi mkuu huru na wa haki mwaka 2017. Viongozi wa CORD pia wamekuwa wakilalamikia
kukataliwa kwa baadhi ya saini zilizowasilishwa na mrengo huo kuunga
mkono ombi la kuandaliwa kwa kura ya maamuzi ya marekebisho ya katiba.
IEBC ilisema saini zilizokuwa halali hazikufika
saini milioni moja zinazohitajika kikatiba ndipo ombi la marekebisho ya
katiba kupitia kura ya maamuzi likubalike.
Post a Comment