0

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF leo July 19 2016 limetangaza kutoa rasmi ratiba ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017, TFF wametangaza kutoa ratiba hiyo ikiwa ni baada ya saa kadhaa kupita toka ianze kuenea ratiba ya Ligi Kuu kuwa imevuja. Ligi itaanza August 31 2016.
Ratiba iliyotolewa na TFF inautofauti na ile iliyosambaa mitandaoni kama imevuja, Ile ya mwanzo imekosewa anwani ya Posta ya TFF na kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon utachezwa August 21, lakini hii rasmi ina anwani sahihi na mchezo huo  utachezwa August 20, 2016.

Post a Comment

 
Top